Magomeni-Coc


Go to content

Gombo Kaya


English | Swahili


Karibu katika tovuti yetu, Kanisa la Kristo-Magomeni, Dar es salaam.


Kanisa ni kundi la watu waliookoelewa na Yesu Kristo mwenyewe kutoka katika nguvu za Shetani (
Wakolosai 1:13-14).

Kanisa la Kristo si madhehebu na halina kiongozi wa kidunia wala makao makuu ya kidunia. Mkuu wa kanisa si mwingine bali ni Yesu Kristo mwenyewe (
Waefeso 1:22-23). Kila kusanyiko la Kanisa la Kristo linajitegemea na tunaunganishwa na Neno la Mungu kwa imani moja (Waefeso 4:3-6)."Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi;"


(Wakolosai 1:13-14)


Tunabarikiwa kwa jina lake Kristo na kwa Roho Mtakatifu Mungu wetu kwa kufuata mafundisho ya Yesu Kristo na Mitume wake na si mafundisho ya wanadamu.

Kanisa la Kristo linawakaribisha wale wote wanaopenda kushiriki nasi kumuabudu Mungu wetu. Tupo hapa kumtumikia Mungu na kukusaidia katika safari yako pamoja na Kristo.

Zingatia: Kanisa la Kristo halina ushirika kwa namna yeyote na madhehebu yeyote yale ya kikristo hata yale yanayojulikana kama "umoja wa makanisa ya kikristo"; Madhehebu si mpango wa Mungu kwa wanadamu (Yohana 17:20-21; 1 Wakorintho 1:10-13).

Ni jambo lililo jema kuhudumu katika Kanisa la Mungu, basi ikiwa tutakuwa na msaada kwako kwa namna yeyote tafadhali usisite kuwasiliana nasi.


Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa anwani ufuatayo:-

Kanisa la Kristo
Magomeni Mwembe Chai
P.O. Box 67632
Dar es salaam
Tanzania

Simu: +255 22 2171532
Fax: +255 (22) ..

Barua Pepe: info@magomeni-coc.or.tz
Tovuti: www.magomeni-coc.or.tz


Mwinjilisti:
+255 763287479


Gombo Kaya | Kuhusu Kanisa | Kusanyiko letu | Anwani za Makanisa | Masomo ya Biblia | Shule ya Biblia | Site Map


Back to content | Back to main menu